•Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametia sahihi mkataba wa maendeleo na Hill-Lewis ambaye ni meya wa Cape Town Afrika Kusini Jumanne 23.
•Sakaja, ambaye kauli yake wakati wa kampeni ilikuwa “wacha tufaifanye Nairobi ifanye kazi”,amekuwa akiendeleza kauli hiyo hasa kwa baraza la kata hiyo kwa kuwapa magari mapya ndipo kufanikisha maendeleo.
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametia sahihi mkataba wa maendeleo na Hill-Lewis meya wa mji wa Cape Town Afrika Kusini.
Sakaja, ambaye kauli yake wakati wa kampeni ilikuwa “wacha tufaifanye Nairobi ifanye kazi”,amekuwa akiendeleza kauli hiyo hasa kwa baraza la Kaunti hiyo kwa kuwapa magari mapya ndipo kufanikisha maendeleo.
Katika mitandao yake ya kijamii alisema kuwa ,“Nina furaha kwa kuusaini mji dada wa Cape Town kwa makubaliano na utawala wa meya Hill-Lewis hivi leo. Nairobi na Cape Town ni majimbo makubwa katika bara letu.”
Sakaja aliendelea na kusema kuwa, kusini na mashiriki mwa Afrika zimeungana pamoja ndipo kuendeleza utendakazi.Haya yanajiri huku baadhi ya vikwazo vilivyoyakumba mataifa haya mawili kuondolewa, ambapo gavana huyo alitaja kama nafasi nzuri kwa watu katika mataifa yote mawili.
“Ushirikiano huu tumeafikiana kuondolewa kwa baadhi ya visa kati ya nchi hizi mbili na ambayo ni nafasi kubwa kwa watu.” Sakaja alisema.